Duniani kuna mambo ya ajabu sana,pengine huwezi hata kufikirikama yanaweza kutokea lakini yapo.Kwa wale ambao hawajui au hawaelewi wanaweza kukataa na kubisha sana lakini hiyo haiondoi ukweli wenyewe.Sote tunafahamu kwamba kuna matukio hujirudia na hii hiutwa sadfa,hii ikimaanisha kwamba tukio moja linaweza kufanana na tukio lingine kwa bahati tu [coincedence].Lakini kuna mfanano ambao kamwe hauwezi kuwa ni kujirudia kwa matukio [sadfa] au tukio kufanana kwa bahati [coincedence]....
Moja kati ya matukio ambayo yamewahi kulela maswali mengi sana katika vichwa vya watu ni tukio la kuzama kwa meli iliyoitwa TITANIC.Je ni kwanini tukio hili liliacha maswali sana vichwani mwa watu? Usipoteze muda,twende pamoja katika makala hii ambapo utaweza kusoma kwa makini matukio mawili kisha nawe utaamua kama ni sadfa,bahati au ni tukio ambalo lilipangwa....
Nitaanza kuelezea tukio la ajali ya Titanic hatua kwa hatua hadi ajali kisha nitaendelea na kile kinachoitwa hadithi ya Futillity...
Karibu sana...
September 17,1908,Liverpoll U.K
Kampuni ya White star line ilitoa oda ya kutengenezewa meli nzuri na ya kifahari kwa wakati ule.Meli ambayo ingekuwa inafanya safari zake kutoka Southampton U.K hadi New York Marekani.Kampuni iliyopewa jukumu la kutengeneza meli hii ilikuwa ni kampuni iliyokwena kwa jina la Harland and Wolff iliyoko Belfast.Meli hii ambayo bajeti yake ni dola mil 7.5 kwa wakati ule ambapo kwa leo ingekuwa ni sawa na dola mil 300.Ilikuwa ni miongoni mwa meli kubwa kabisa kwa wakati ule na meli ghali zaidi...
Utengenezaji au uundwaji wa meli
Utengenezaji wa meli ulianza ramsi tarehe 31 May 1909 na kukamilika tarehe 2 April 1912.Titanic ilikuwa ni miongoni mwa meli kubwa tatu za kampuni ya White Star Line na meli zote zilitengenezwa mjini Belfast,Irland na kampuni maarufu ya wakati huo Harland and Wolff iliyokuwa maarufu sana kuanzia miaka ya 1867.
Utengenezaji wa Titanic mwaka 1909
Titanic ilikuwa na urefu wa futi 882 na mita 9 ambayo ni sawa na mita 269.06.Idadi ya abiria ambao waliweza kuwepo kwenye daraja la kwanza ni 833,daraja la pili ni 614,na daraja la tatu ni 1006 ambayo idadi ya abiria wote ni 2453.Meli hii ilikuwa na uwezo wa kubeba wafanyakaji wa meli 900.Kwa maana hii meli hii ilikuwa na uwezo wa kubema watu 3,547.Ilikuwa na boti kwaajili ya dharula 20 ambazo zilikuwa na uwezo wa kubeba watu 65 kila moja.....
Titanic yakamilika na yaondoka Belfast
Siku ya jumanne tarehe 2 April 1912 saa 6.00 A.M meli hii ya Titanic ilianza safari yake ya kwanza kabisa kwenye maji ikitokea Blefast kuelekea Southampton kwaajili ya kuanza safari yake ya kwanza ya kikazi.Safari hii ilichelewa kwa siku moja kutokana na ubovu wa hali ya hewa.Siku hii ndiyo meli hii ilifanyiwa majaribio kwa namna tofauti na wataalam walioitengeneza ikiwa njiani kuelekea Southampton.Ilijaribiwa namna ya kasi yake na uwezo wake wa kukata kona pamoja na mengine mengi....
Meli hii ilisajiliwa Liverpool kuwa kama ndiyo bandari ya nyumbani lakini safari zake zilikuwa ni kutoka Southampton kuelekea New York kutokana na jiografia ya eneo husika na ukubwa wa meli.
Safari ya kwanza na ya pekee ya Titanic
Siku ya safari yake ya kwanza meli ya Titanic ilikuwa ni tarehe 10 April 1912 kuelekea Nwe york na ilikuwa na wafanyakazi 885.Kiongozi wa meli hii alikuwa akiitwa Cpt.Edward John Smith pamoja na msaidizi wake ambaye aliitwa Henry Tingle Wilde.Katika wafanyakazi wote wanawake walikuwa ni 23 pekee na wengine walikuwa ni wanaume na wengi walikuwa kwaajili ya kuwahudumia abiria na wachache walikuwa ni wataalamu wa injini na mambo mengine kama moto n.k....
Idadi ya abiria..
Abiria walikuwa ni 1317,;324 katika daraja la kwanza,284 katika daraja la pili na 709 katika daraja la tatu.Kati ya hao 869 walikuwa ni wanaume,447 walikuwa ni wanawake na watoto walikuwa ni 107.Siku hii ya safari ambayo ilikuwa ni April 10,1912 watu walianza kuingia kwenye meli saa 9:30 za asubuhi na safari ilianza majira ya alasiri.
Meli ilianza safari yake kuelekeaCherbourg, Ufaransa ikiwa ni moja kati ya maeneo ambayo ilipaswa kupitia ikielekea Yew York Marekani.Kutoka Southampton hadi katika bandari ya Cherbourg,Ufaransa ni kilomita 143.Siku hii hali ya hewa ilikuwa nzuri lakini yenye baridi kali.Kutokana na bandari ya Cherbourg kuwa na nafasi ndogo ya kupokea meli kubwa kama Titanic,meli hii ililazimika kuwahamishia wasafiri kwenye meli ndogo ili wamalizie safari zao na kampuni iliyokuwa inamiliki meli ya Titanic ilikuwa na meli mbilia ndogo ambazo ni SS Traffic na SS Nomadic ambazo zilikuwa zikifanya kazi Ufaransa na ndizo zilizotumika kusafirisha abiria kutoka kwenye meli ya Titanic hadi bandarini Cherbourg....
Baada ya masaa manne,baada ya kuondoka kwenye bandari ya Southampton meli ya Titanic iliwasili katika pwani ya Cherbourg.Meli ndogo ambazo zilipaswa kupokea abiria kwaajili ya kuwapeleka bandarini Cherbourg kutokana na meli ya Titanic kuwa kubwa na kushindwa kufika hapo bandarini ziliwasili ilipokuwa imesimama meli kuwa na ya kuvutia kabisa,meli ya Titanic.Abiria waliteremka kutoka kwenye meli hii kubwa na kuingia kwenye meli ndogo lakini pia kulikuwa na abiria waliokuja kupanda meli ya Titanic kutoka Ufaransa kwaajili ya kuelekea Marekani.Titanic ilipokea abiria wapya 247 na zoezi la kubadilishana abiria lilitumia dakika 90 na majira ya saa 8:00 usiku safari ya kuelekea Marekani ilianza kutokea hapo Cherbourg Ufaransa....
Saa 11:30 asubuhi meli hii ya kuvutia iliwasili katika pwani ya Cork Harbour iliyokuwa kusini mwa nchi ya Ireland katika jiji la Queenstown.Eneo hili ilikuwa na mawingu lakini ya joto.Kama ilivyokuwa Ufaransa,bandari ya eneo hili nayo ilikuwa ndogo kuweza kupokea meli kubwa kama Titanic na utaratibu kama ule ule ulitumika Cherbourg wa kushusha abiria ambapo pia abiria wengine walishuka na wengine kupanda.Hapa Titanic ilipokea abiria wengine wapya 123....
Meli hii ilitarajiwa kufika New York asubuhi ya tarehe 17,1912.Iiondoka Ireland katika jiji la Queenstown ikianza safari yake ya kuikatiza bahari ya Atlantic.Iliondoka katika pwani ya Ireland kukiwa na hali ya joto na mawingu ambayo haikuwa hali yenye kutia mashaka yoyote kwa meli hii ya kuvutia.Hali ya hewa ilibakia kuwa ya namna hiyo hadi tarehe 13 April ambapo ilibadilika na kuwa ya baridi kali huku safari ikiendelea.Katika eneo hili la bahari meli ilikumbana na upepo mkali kiasi ambapo ulikuwa na baridi kali sana.Hali hii iliendelea hadi jumapili ya tarehe 14,1912 ambapo hali ya hewa ilikuwa imetulia lakini yenye baridi kali...
Kufikia hapa walikuwa wameshatembea siku tatu kutokea pwani ya jiji la Queenstown,Ireland bila tatizo lolote.Kitu ambacho abiria hawakuelezwa ni kwamba chini kwenye injini kulikuwa na moto uliokuwa unawaka tangu wakiwa katika bandari ya Southampton na safari iliendelea moto huu ukiendelea kuwaka huku wataalam wa kuzima moto ule wakiendelea kuhangaika kuuzima lakini bahati nzuri moto huu ulizimika siku hii ya tarehe 14....
Eneo la ajali..
Meli ya Titanic ikawa imeingia katika eneo la kaskazini mwa mji wa Newfoundland katika bahari ya Atlantic na kufikia hapa ilikuwa imeshatembea umbali wa kil zaidi ya 400 kutokea ilipoanza safari zake...
Siku hii ya tarehe 14 meli ya Titanic ilipata taarifa ya kuonywa juu ya kuwepo kwa mabonge makubwa ya barafu yaliyokuwa yakielea baharini.Meli ya kwanza kuionya Titanic ilikuwa ni meli iliyokuwa na jina la Mesaba.Lakini wafanyakazi wa Titanic hawakujali na waliendelea kukimbia kwa kasi ile ile ambayo ilikuwa ni kubwa sana ambapo ilikuwa inakimbia speed ya kil 39 kwa saa...
Meli iliendelea na safari yake na tahadhari haikuchukuliwa kutokana na imani zilizokuwa zimeenea sana wakati ule kwamba barafu zilizokuwa zinaelea baharini hazikuwa na hatari kwa meli kubwa kama Titanic....
Hatimaye saa 11:30 usiku wa April 14 1912,mmoja wa wafanyakazi wa meli ile anayekwenda kwa jina la Frederick Fleet aliona bonge kubwa la barafu likielea kuelekea ilipo meli ya Titanic.Haraka sana alitoa taarifa hii kwa afisa mmoja wa meli aliyekuwa ndani ya meli aliyeitwa William Murdoch na baada ya kupokea taarifa hii afisa huyu aliagiza injini ya meli izimwe na aliagiza meli iizunguke barafu ile kwa kukata kona ya haraka sana.Lakini walikuwa wamechelewa na barafu iliigonga meli hii pembeni na kusababisha matundu makubwa sana na ya hatari mahali ambapo maji ndiyo sehemu yake ya kugonga kwenye meli pembeni chini....
Maji yalianza kuingia kwenye meli kwa kasi ya hatari kabisa na kuamsha hofu miongoni mwa mafundi wa meli ile.Walianza kujaribu kufikiria namna ya kukabiliana na hatari hii bila kuwajulisha abiria bila mafanikio yoyote na taratibu meli ilianza kuzama kwa nyuma.Meli ilikuwa na makoti maalum kwaajili ya kuogelea ambayo yaliwatosha nusu tu ya abiria waliokuwa ndani ya meli kwa wakati ule....
Baada ya kushindwa cha kufanya na kuona kuwa abiria wataanza kuona kuna hali isiyokuwa ya amani kwenye meli,ilibidi waelezwe kilichotokea na wakaambiwa ukweli kuwa makoti maalum ya kuogelea hayakutosha.Waliambiwa kuwa watakaoanza kupewa makoti hayo ni watoto kwanza kisha wanawake na waliagizwa wajipange mstari.Hali hii ilizua tafrani kubwa na wengine walianza kuchanganyikiwa kwa namna ya hatari...
Ilipofika saa 2:20 usiku yaani masaa mawili na dakika 40 baada ya meli kugonga barafu,yaani saa nane na dakika ishirini meli iliongeza kasi ya kuzama na kusababisha ianze kuinuka upande mmoja.Kadiri kasi ya maji kuingia ndani ya meli ilivyozidi ndipo meli nayo iliongeza kasi ya kuzama.Watu walikuwa wakipewa makoti maalum ya kuogelea huku wengine wakiwa na taharuki kubwa.Watoto walikuwa wakiwekwa kwenye boti maalum za dharula pamoja na wanawake na wengine walikuwa wameshaondoka kwenye meli na walikuwa wakiishuhudia namna inavyozama huku ikiwa na wapendwa wao ndani....
Watu walikuwa wakilia na wengine wakijaribu kutafakari namna ya kufanya.Kundi la kwanza la watoto na wanawake waliokuwa kwenye boti ya kwanza maalum kwaajili ya dharula ambayo waliwekwa humo na kuondolewa kwenye meli ya Titanic walikuwa wakiiangalia meli huku wakilia kuwalilia wapendwa wao waliowaacha kwenye meli iliyokuwa ikiendelea kuzama.Taa za kwenye meli zilikuwa zikionekana kuzama upande mmoja huku upande mwingine zikionekana kunyanyuka juu....
Maji yaliendelea kuingia kwenye meli na kwa kihoro kikubwa sana walishuhudia meli ikikatika katikati kutokana na kuzidiwa kwa uzito eneo moja na hatimaye meli iliongeza kasi ya kuzama.Hatimaye meli ilizama kwenye maji na kupotelea yote ikiwa pamoja na kiongozi wa meli hiyo Cpt.Smith.Abiria wengi walijikuta wakiwa kwenye maji yaliyokuwa na baridi kali ya -2c ambapo wengi walifariki kwa baridi kali....
Hatimaye historia ya meli hii iliishia siku hii ya usiku wa alfajiri ya kuamkia tarehe 15 April mwaka 1912.Meli ya kwanza kufika kwenye eneo la ajali ilikuwa ni RMS Carpathia majira ya alfajiri ya saa 4:00.Watu 866 waliokolewa kutoka kwenye ajali hii mbaya kabisa kupata kutokea...
Gazeti la New York times likiandika habari za kuzama meli hiyo tarehe 15 April 1912...
Watu waliokadiriwa kufika au kuzidi 1500 walipoteza maisha katika ajali hii mbaya kabisa....
Mwaka 1997 tukio hili la kusikitisha lilitengenezewa filamu ambapo wacheza filamu Kate Winslet na Leonardo Di Caprio walicheza humo na filamu hii ilifanya mauzo ya kutisha kabisa..